Kumuoa mjane kwa kumuonea huruma na kutaka kumsaidia

Swali: Mimi nataka kumuoa mjane kwa kumuonea huruma kwa sababu ni mjane na ni masikini. Lakini watu hawakunishauri naye na wamenambia nisimuoe kwa kuwa wanaona kuwa kitu chenye kumtia kasoro. Je, nimuoe au hapana?

Jibu: Ikiwa mwanamke huyu kuna chenye kumtia kasoro upande wa dini au tabia yake sikushauri umuoe. Ikiwa hiki chenye kumtia kasoro hakimtii kasoro upande wa dini wala tabia hakuna neno kumuoa. Lakini unatakiwa kuchunguza kwanza mambo yambainikie. Kwa sababu huenda akafikiria kasoro alionayo ni ndogo kumbe ni kubwa zaidi ya vile alivyokuwa anafikiria. Huu ndio upambanuzi katika mambo haya. Kasoro ikiwa inahusiana na tabia na dini hatakiwi kumuoa wala asisogee karibu naye. Lakini ikiwa inahusiana na kitu kingine ni sawa akamuoa. Lakini anatakiwa kumtazama kwanza ili awe juu ya ujuzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (12) http://binothaimeen.net/content/6760
  • Imechapishwa: 19/12/2020