Swali: Nikiandika kitabu na kunuia thawabu zimwendee mama yangu ambaye kishakufa – Allaah amrehemu. Je, kitendo hichi kinajuzu?

Jibu: Ni sawa. Ikiwa kitabu hicho ni chenye kuwanufaisha watu na hakikutanguliwa [kuandikwa hapo kabla], hichi ni kitendo chema. Huku ni kueneza elimu. Ama ikiwa ni kile kile kinachoandikwa na hakuna jipya, bora zaidi nunua vitabu na ufanye Waqf kwa mama yako. Hili ni bora zaidi kuliko kujitaabisha kwa kutunga kitabu ambacho tayari kipo na kusiwe jipya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (64) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-02.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020