Kumtumia mbwa mwitu wakati wa matabano

Swali: Ni jambo limeenea kwa watu wa kawaida na kwa baadhi ya wasomaji wanapojiliwa na mtu ambaye amepatwa na jini wanamleta mbwa mwitu kisha wanasema kuwa ni jambo limethibiti kwao kwa uzoefu kwamba ambaye amepatwa na jini anapoona mbwa mwitu basi jini huyo hutoka, jambo ambalo limeshuhudiwa kutoka kwa watu wenye kuaminika. Wanasema kuwa hawana imani fulani kwa mbwa mwitu huyo, lakini ni jambo ambalo linatokana na desturi katika matibabu kwa uzoefu na kwamba imethibiti kuwa mbwa mwitu anamtoa jini.

Jibu: Ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Msingi katika matibabu ni kwamba inafaa kuyatumia yale mambo yote ambayo yameruhusiwa muda wa kuwa yamejaribiwa na yananufaisha. Huu ndio msingi katika matibabu. Ni jambo ambalo wanalidai kwamba humkimbiza mbwa mwitu na kwamba mbwa mwitu humtoa jini kwa mtu pale anapomuona, jambo ambalo linapelekea kuwa na imani fulani kwa mbwa mwitu huyo na hivyo wakaning´iniza ngozi yake – kama yanavofanywa na baadhi ya watu – au wakaning´iniza kichwa chake.

Mimi naona kuwa inatakiwa kuacha jambo hilo ili kusitokee maafa watu wakaanza kuwa na imani fulani juu ya mbwa mwitu na kwamba wanasababisha kuwatenga mbali majini. Mara nyingi haya yanakuwa ni ukhurafi miongoni mwa mambo ya ukhurafi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23767/حكم-زعم-ان-الجن-ينفر-عند-روية-الذىب
  • Imechapishwa: 23/04/2024