Baadhi ya maswali kuhusu uinuaji wa macho juu wakati wa kuswali

Swali: Hadiyth iliotangulia:

“Watakoma kufanya hivo au yatapofolewa macho yao.”

inabainisha kuwa inafaa kutazama mbele ya mswaliji?

Jibu: Kunapohitajika kufanya hivo.

Swali: Swalah inabatilika kwa kutazama juu?

Jibu: Hapana, haibatiliki. Hata hivyo analazimika kutubia kutokana na hilo. Haijuzu kwake kufanya hivo.

Swali: Hapa amesema:

“Akiwa mbele ya Ka´bah ni bora kuitazama yenyewe kuliko kutazama mahali pa kusujudia.”?

Jibu: Sijui kuthibiti kwa jambo hilo. Sunnah ni kuinamisha macho na unyenyekevu.

Swali: Makatazo si yanapelekea uharibikaji?

Jibu: Hapana, makatazo ya kuinua macho hayaharibu swalah. Hata hivyo imekatazwa kuinua macho.

Swali: Matishio si yanafahamisha kuharibika kwa swalah?

Jibu: Ni matishio ya kupofolewa macho. Tunamuomba Allaah usalama.

Swali: Je, imepokelewa jambo linalojulisha kuwa inatakiwa kutazama mahali pa kusujudia?

Jibu: Udhahiri ni kwamba ni jambo limechukuliwa kutoka katika yale maamrisho ya kunyenyekea na kutoinua macho. Vinginevyo ni jambo hatujafahamishwa kutoka katika maneno ya wanazuoni.

Swali: Je, swalah inasihi, licha ya kwamba inachukiza, ikiwa mtu anainua macho yake juu?

Jibu: Hiki ndicho kinadhihiri. Swalah inasihi kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuamrisha kuirudia na wala hakusema kuwa imebatilika. Alichowafanya ni kuwakataza tu kuinua macho yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23755/حكم-رفع-البصر-الى-السماء-اثناء-الصلاة
  • Imechapishwa: 23/04/2024