04 – Kila mmoja wa wanandoa amtosheleze mwengine ile starehe zilizowekwa katika Shari´ah

Kwa mapenzi, ukunjufu wa uso, maneno mazuri na kila mmoja wa wanandoa ayapupie hayo.

Kwa mfano mwanamke anahitaji kuambiwa maneno mazuri na kufanyiwa huruma na mume wake. Asipoyasikia kutoka kwa mume wake pengine kuna khatari shaytwaan akamchezea na akayasikia kutoka kwa mtu wa kando naye na hivyo akaangamia. Hakika tuna ruwaza njema kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akicheza na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa), akimfanyia mzaha na akifanya naye mashindano[1].

”Alikuwa akiweka kichwa chake kwenye mapaja yake naye yuko na hedhi.”[2]

Ameipokea Ahmad.

Mpaka wakati wa jimaa mume anapaswa kutambua adabu zake.

Ibn-ul-Qayyim amesema katika ”at-Twibb an-Nabawiy”:

”Miongoni mwa vitu vinavyotakiwa kutangulizwa kabla ya jimaa ni kumchezesha mwanamke, kumbusu na kumnyonya ulimi wake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwachezesha wakeze na akiwabusu.”

Abu Daawuud amepokea katika ”Sunan” yake ya kwamba alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimbusu ´Aaishah na akimyonya ulimi wake[3].

Inatajwa kwamba Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kumwingilia kabla ya kucheza[4].”[5]

[1] Abu Daawuud (2578). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Abiy Daawuud” (6363).

[2] Ahmad katika ”al-Musnad” (40/494) (64435).

[3] Abu Daawuud (2386). Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Abiy Daawuud” (515).

[4] Zaad-ul-Ma´aad (04/253). al-Albaaniy amesema kuhusu Hadiyth hii ya Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh):

”Imetungwa.” (Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´ (6056))

[5] at-Twibb an-Nabawiy, uk. 196

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 24/04/2024