Swali: Mwanaume wa Kiislamu akimtukana mke wake au Dini yake anakuwa ni mwenye kutalikika Kishari´ah kama tunavyosikia kwa watu wengi?
Jibu: Akimtukana mke wake hatalikiki. Lakini ni juu yake atubu kwa Allaah na apatane na mke wake. Na ikiwa watasameheana, hakuna kitu. Na ikiwa atamtusi kama (mke) alivyomtusi kwa kulipiza kisasi bila ya kuzidisha juu ya hilo, haina neno. Na ikiwa atamsamehe ndio bora zaidi. Kwa kuwa Allaah Anasema:
اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ
“Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa.” (05:08)
Ama kumtukania Dini yake ilihali naye (mwanamke huyo) ni Muislamu, huu ni ukafiri. Tunamuomba Allaah afya. Ikiwa mume ni Muislamu na mke ni Muislamu, kutukana Dini yake ina maana kautukana Uislamu. (Mke) asiishi naye (huyo mume). Atiwe adabu (huyo mume) na apigwe kwa kitendo chake hichi kibaya na aambiwe kutubia.Akitubu kwa kitendo chake hichi kibaya (ni vizuri) la sivyo ni wajibu (mume huyo) kuuawa. Ni wajibu kwa mtawala wa Waislamu au kiongozi wa nchi wamfanye atubu, la sivyo auawe. Kwa kuwa kutukana Dini ya Kiislamu ni katika aina mbaya kabisa za ukafiri zinazovunja Uislamu (wa mtu). Hali kadhalika kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutukana Qur-aan.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
- Imechapishwa: 25/03/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related

Mume na mke wanatofautiana katika masuala ya dini
https://www.youtube.com/watch?v=__6wloB28-o Swali: Mke katofautiana na mume wake katika jambo la Shari´ah. Yeye mke anaamini kuwa ni Haramu na mume anaamini kuwa inaruhusiwa. Mume anamuamrisha kukifanya. Je, mke amtii? Jibu: Ikiwa kafikia daraja ya Ijtihaad, atakuwa ni mwenye kufanya ´Ibaadah kwa ufahamu wake na Ijtihaad yake. Ama ikiwa ni mwanamke anayefuata matamanio…
In "Elimu na masomo"
Nimtaliki mke ambaye haswali?
Swali: Mimi nimeoa na nina watoto watatu na mimi natendea kazi dini ya Uislamu – Allaah akitaka. Mke wangu ni muislamu ambaye anafunga Ramadhaan. Lakini haswali, hafanyi chochote na wala hanyenyekei kutekeleza swalah. Je, nina haki ya kumtaliki kwa mujibu wa Shari´ah ikiwa hanitii? Jibu: Ikiwa mke wako haswali na…
In "Ibn ´Uthaymiyn kuhusu hukumu ya swalah"

Kamtaliki mke wake kwa kwenda jirani bila ya idhini yake
https://www.youtube.com/watch?v=SA0rtCCJNYA Swali: Mke wangu alienda kwenye nyumba ya jirani mmoja nikakariri kumtaliki kwa sababu ya kwenda kwake bila ya idhini yangu. Nikamwambia chukua kila chako kwenye nyumba hii na mimi ni haramu kwako. Lakini wazazi wangu wawili hawakukubaliana na mimi, wakanambia: "Wewe ndiye utatoka kwenye nyumba hii na yeye (mke…
In "Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz"