Swali: Mimi nimeoa na nina watoto watatu na mimi natendea kazi dini ya Uislamu – Allaah akitaka. Mke wangu ni muislamu ambaye anafunga Ramadhaan. Lakini haswali, hafanyi chochote na wala hanyenyekei kutekeleza swalah. Je, nina haki ya kumtaliki kwa mujibu wa Shari´ah ikiwa hanitii?

Jibu: Ikiwa mke wako haswali na anaacha swalah na ni mwenye kuendelea juu ya kuacha swalah, basi ni kafiri. Haya ndio maoni yenye nguvu miongoni mwa maoni ya wanachuoni ya kwamba mwenye kuacha swalah ni kafiri. Inahusiana na kufuru kubwa yenye kumtoa mtu nje ya Uislamu. Kujengea juu ya haya mwanamke huyo ni haramu kwako mpaka pale ataporudi katika dini yake na kuanza kuswali. Haijuzu kwako kumbakiza kwako katika hali hii. Kwa sababu ndoa yake imefutika kwa kuritadi kwake. Isipokuwa akitubia, akarudi katika dini ya Uislamu na akaanza kuswali. Hapo ndipo atakuwa mke wako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (07) http://binothaimeen.net/content/6710
  • Imechapishwa: 08/11/2020