Swali: Je, inafaa kumtukana kafiri kwa dhati yake?

Jibu: Ni sawa pale inapozidi shari yake. Ni kama ambavo Mtume alimwombea du´aa mbaya Abu Jahl, Swafwaan bin Umayyah na kundi la watu wengine pale yalipozidi maudhi yao.

Swali: Vipi kuhusu muislamu mtenda dhambi nzito?

Jibu: Haitakiwi kumtukana muislamu mtenda dhambi kwa dhati yake; mfano aseme kwamba Allaah awalaani madhalimu, Allaah awalaani mafasiki, Allaah awalaani wezi na kwamba Allaah awalaani wazinzi. Lakini asimtukane mtu mmoja mmoja kwa dhati yake. Hivo ndio bora. Wako wanazuoni wanaojuzisha hivo, hata hivyo bora ni kutotukana mtu mmoja mmoja kwa dhati yake. Pengine Allaah akamwongoza. Kunatarajiwa kwake kuongoka. Kwa hivyo kuacha kumtukana mtu mmoja mmoja kwa dhati yake ndo bora. Isipokuwa yakizidi maovu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtukana Abu Jahl na kundi la watu wengine kutokana na maudhi yao makubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24314/هل-يجوز-سب-الكافر-والفاسق-بعينه
  • Imechapishwa: 28/09/2024