Kumswalia Mtume wakati wa kuandika jina lake

Swali: Je, ni lazima kuandika “Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam” wakati anapotajwa katika maandishi?

Jibu: Ndio yenye kudhihiri wakati anapotajwa na wakati unapomsikia. Wakati anapoandikwa na wakati unampomsikia akitajwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh:

”Liguse mchanga pua la yule ambaye nitatajwa mbele yake na asiniswalie.”

Jibriyl alimwambia:

”Liguse mchanga pua la mja ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie.” Sema: ”Aamiyn.” Nikasema: ”Aamiyn.”[1]

Haya yanajulisha kuwa ni wajibu.

Swali: Vipi ikiwa mtu ataandika “Mtume” kisha akamswalia kwa mdomo na asiandike?

Jibu: Yanafikiwa malengo. Hata hivyo bora aiandike ili amsaidie pia yule msomaji.

[1] Cheni ya wapokezi wake ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy” (18).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23003/حكم-كتابة-الصلاة-والتسليم-لذكر-النبي-ﷺ
  • Imechapishwa: 07/10/2023