Swali: Ambaye anaswali sunnah na kukatajwa jina la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amswalie?

Jibu: Akipitia jina la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kisomo chake ndani ya swalah amswalie kwa siri. Ama akimsikia mtu nje ya swalah anamtaja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asimswalie ndani ya swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-25.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020