Hadiyth ya mwanamke kutosafiri bila Mahram inahusu usafiri wa kila aina na kila zama

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kusafiri peke yake kutoka Jeddah kwenda Riyaadh kwa kuwa mume wake anaishi Riyaadh na yeye anasoma Jeddah pamoja na kujua pia muda wa safari yake kwa usafiri wa ndege ni saa moja au saa moja na nusu?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Wewe unasema kuwa ni halali kwake ilihali Mtume anasema kuwa si halali? Hili halijuzu. Asisafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram, sawa usafiri wa ndege, gari, mnyama, kwa kutembea na kadhalika. Hadiyth iko kwa jumla. Hakuweka mpaka njia ya usafiri maalum. Hadiyth inahusu kila zama na kila pahali.

Mahram ana maslahi kwa mwanamke na ni mwenye kumlinda, sawa kwenye ndege na kwenginepo. Tusiende kinyume na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa upuuzi wa kwamba ni safiri fupi, mwanamke yuko na kundi la watu na mfano wa hayo na huku twende kinyume na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Hii haikufungwa [Mutlaq]. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuvua kitu. Mwanamke anahitajia Mahram, sawa akiwa ndani ya ndege, gari, kundi n.k. Je, kwani hilo kundi la watu ni Mahram zake? Hapana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-25.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020