Kumswalia maiti kaburini kwa yule aliyepitwa na swalah ya jeneza

Swali: Ni ipi hukumu ya kumswalia maiti naye yumo ndani ya kaburi pamoja na kujua ya kwamba yule anayetaka kumswalia ameshamswalia kabla ya kuzikwa?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswalia kaburi la mwanamke ambaye alikuwa anausimamia Msikiti [kwa usafi] na akafa usiku. Wakamwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu kufa kwake na hakuwepo, hivyo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaenda na wakamuonesha mahali lilipo kaburi lake na akamswalia. Kuliswalia kaburi kwa yule ambaye amepitwa na Swalah ya jeneza kabla ya kuzikwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ama kuhusiana na mtu ambaye ameshamswalia kabla ya kuzikwa, hii inatosha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_08.mp3
  • Imechapishwa: 01/06/2015