Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kumwita mtoto wake “Hizb-ul-Llaah” (kundi la Allaah)? Baba yangu amenipa jina la Hizbu-ul-Llaah na nimefikisha umri wa miaka 29 na nafanya kazi ya utabibu. Nimesikia kuwa jina hili linachukizwa. Je nibadilishe jina langu?

Jibu: Jina hili ni geni. Hizb-ul-Llaah ni watu wa utiifu na Imani:

أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.” (58:22)

Hizb-ul-Llaah ni watu wa utiifu na Imani na Taqwa. Wewe ikiwa ni katika watu wa Imani, basi ni katika Hizb-ul-Llaah. Ikiwa ni kinyume na hivyo, basi sio katika Hizb-ul-Llaah. Ukilibadilisha ni bora. Badilisha badala ya Hizb-ul-Llaah ´Abdullaa. Ni jina zuri. ´Abdullaah, ´Abdur-Rahmaan, ´Abdul-Kariym, ´Abdul-Maalik na mfano wa hayo. Haya ni majina mazuri. Kwa kuwa kuitwa kwa jina la Hizb-ul-Llaah kunaweza kuwa ndani yake kitu kama Tazkiyah (kujitakasa) ilihali wewe hujui ni miongoni mwa Hizb-ul-Llaah au hapana? Hili ni jambo la khatari. Ukilibadilisha kwa ´Abdullaah au ´Abdur-Rahmaan ni bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12822
  • Imechapishwa: 03/05/2015