Mwanamke kuswali na nguo ya kulalia

Swali: Mwanamke akiswali na nguo ambayo ni kanzu ya kulala nayo Swalah yake ni batili?

Jibu: Ikiwa inasitiri, hata kama itakuwa ni kanzu ya kulalia, Swalah yake ni sahihi. Mwili wa mwanamke wote ni ´Awrah. Ikiwa inasitiri mwili na kusionekane isipokuwa uso, Swalah yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12822
  • Imechapishwa: 03/05/2015