Haijuzu kushirikiana na Ahl-ul-Bid´ah kwa madai ya kuwalingania

Swali: Je, inajuzu kwa mwenye kudai elimu kuwatolea mawaidha watu na kuwaelekeza na kukusanyika kwenye jeneza na kushirikiana na watu katika Bid´ah zao ili ya kuwatolea mawaidha na kuwanasihi kama jinsi anavyodai?

Jibu: Kushiriki katika Bid´ah kwa njia ya kunyamazia na kuridhia, haijuzu. Ama akienda sehemu ya Bid´ah ili kuwakumbusha na kutahadharisha kisha akawaacha pasina kushirikiana nao, hakuna neno. Akienda sehemu ya Bid´ah ili kuwatahadharisha dhidi ya Bid´ah – kwa kutumia fursa hii ya kukusanyika kwao – hili halina neno. Ama kushirikiana nao katika kusherehekea kwao na kudai kuwa anawatahadharisha, hapana. Huku sio kukataza. Awakataze na kuwatahadharisha na ajiweke mbali na kushirikiana nao katika Bid´ah. Hili ndilo la wajibu kwa kila mwenye elimu pale atapowatahadharisha watu kutokana na Bid´ah na kuwakataza Bid´ah wazifanyazo na atengane nao na wala asiwe pamoja nao na kushirikiana nao.

Swali: Wala asile nao hata maulidini?

Jibu: Asile kwenye maulidi. Kinyume chake awatahadharishe na kujitenga nao na awakataze.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12822
  • Imechapishwa: 03/05/2015