Kumnyonyesha mtoto wa miaka kumi aliyeokotwa

Swali: Nilienda katika nyumba ya watoto waliookotwa na kumtunza mtoto wa kile mmoja katika wao ambaye alikuwa na mwaka mmoja. Hivi sasa msichana huyo yuko na miaka kumi na anazingatiwa ni mmoja katika wanafamilia. Nasumbuka kwa kule kuchanganyikana kwake na watoto wangu wa kiume na kulazimika kwake kujisitiri mbele yao. Nimesikia kwamba ufumbuzi ni mke wangu amnyonyeshe mara tano na baada ya hapo atakuwa ni mwana wetu wa kunyonya…

Jibu: Fatwa hii ni ya makosa. Huku ni kumnyonyesha mtumzima. Wanazuoni wengi wanaona kuwa kumnyonyesha mtumzima hakuharamishi chochote. Kwa hivyo fatwa hii ni ya kimakosa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 27/02/2022