Kumlisha masikini mmoja kutokana na idadi ya masiku yanayolazimikia mtu

Swali: Inatosheleza kwa mtu juu ya zile idadi za swawm ikiwa atampa chakula masikini mmoja?

Jibu: Haikutoshelezi kwa mtu juu ya masiku mengi akampa chakula masikini mmoja. Kwa kuwa kila siku anatakiwa kumlisha masikini. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

”Wale wanaoiweza lakini kwa uzito, basi walishe masikini.” (02:284)

Ni lazima awalishe masikini kiasi cha idadi ya masiku yaliyo juu yake. Lau atalisha masikini mmoja wawili ilihali juu yake inamlazimikia masiku kumi, haitoshelezi. Lau atalisha masikini tisa, ni lazima akamilishe masikini kumi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 01
  • Imechapishwa: 23/09/2020