Swali: Uwajibu wa kulisha unadondoka lau ikiwa mtu atamlisha chakula mtoto au kafiri?

Jibu: Kauli sahihi ni kwamba anayekula chakula haina neno akalishwa [mtoto]. Kuhusu kafiri haijuzu akalishwa katika kafara. Kwa kuwa kafara imeshurutishwa anayeipewa awe ni katika Waislamu.

Lakini hata hivyo, kuhusu zakaah ni jambo pana zaidi kwa kuwa inajuzu kumpa kafiri anayetiwa nguvu juu ya Uislamu. Ama kuhusu mambo ya kafara, kafara ya swawm, yamini na mume kumfananisha mke na mama yake hakudondoshi wajibu wake lau atapewa nayo kafiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 01
  • Imechapishwa: 23/09/2020