Kumhimidi na kumshukuru Allaah baada ya kuchemua

Swali: Je, imesuniwa kwa mwenye kuchemua kusema:

الحمد لله و الشكر لله

”Himdi zote njema na shukurani anastahiki Allaah.”?

Jibu: Inatosha kusema:

الحمد لله

”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Himdi ndio shukurani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 19/07/2024