Amempata mtoto wake mchanga amekufa kitandani

Swali: Mwanamke alilala kitandani na mtoto wake mchanga. Wakati alipoamka akamkuta kuwa ameshakufa na anakhofia labda alimlalia na akafa kwa sababu hiyo. Je, analazimika kutoa kafara kwa jambo hilo?

Jibu: Hapana. Haikuthibiti kuwa alimlalia. Wala haikuthibiti kuwa amekufa kutokana na sababu hiyo. Kwa vile haikuthibiti hakuna kinachomlazimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (45)
  • Imechapishwa: 19/07/2024