Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu mwanamme kumgusa kwa mkono mwanamke asiye Mahram wake pasi na kizuizi – kunachengua wudhuu´?

Jibu: Kumgusa mwanamke hakuchengui wudhuu´ kwa hali zote kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliwabusu baadhi ya wakeze kisha akaswali na hakutawadha.

Haifai kwa mwanamke kupeana mkono na mwanamme yeyote asiyekuwa Mahram wake. Pia haifai kwa mwanaume kupeana mkono na mwanamke asiyekuwa Mahram wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi sipeani mkono na wanawake.”

Pia kutokana na yale yaliyothibiti kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaahidi utii wanawake kwa maneno peke yake.” ´Aaishah amesema: “Hakupatapo hata siku moja kugusu mkono wa mwanamke.”

Allaah (Subhaanah) amesema:

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا

“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah kwa yule mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho na akamtaja Allaah kwa wingi.”[1]

Wanamme kupeana mkono na wanawake na wanawake kupeana mkono na wanamme wasiokuwa Mahram zao ni miongoni mwa sababu za fitina zote. Shari´ah ya Kiislamu imekuja kuziba njia zote zinazopelekea katika yale aliyoharamisha Allaah.

[1] 33:21

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/133)
  • Imechapishwa: 22/08/2021