Kumfanya mume wa dada kuwa Mahram

Swali: Ni ipi hukumu mwanamke kumfanya mume wa dada yake kuwa Mahram yake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamme hakai chemba na mwanamke yeyote isipokuwa shaytwaan huwa ni watatu wao.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Unaonaje Hamuu?” Akasema: “Hamuu ni kifo.”

Hamuu ni kaka yake mume. Huyu ni uduyuthi ambapo mke wa mtu akapigiwa simu na ambaye si Mahram yake. Moyoni mwake hamna wivu juu ya mke wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Waqafaat ma´aa Hadiyth tatadaa´ alaykum-ul-Umamu https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-09/wgfaaat.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2022