Kumekimiwa swalah ya faradhi baada ya kubaki Rak´ah moja ya Sunnah

Swali: Je, kama kumebaki Rak´ah moja ya Raatibah mtu aikate swalah yake?

Jibu: Ndio, aikate. Isipokuwa ikiwa kama ameshaenda Rukuu´ ya pili amalize swalah yake.

Swali: Baadhi yao wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunapokimiwa swalah basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile ya faradhi.”

Hakusema:

“Kunapokimiwa swalah basi hakuna sehemu ya swalah isipokuwa ile ya faradhi.”

Yeye hivi sasa anaswali sehemu ya swalah iliyobaki.

Jibu: Rak´ah huitwa kuwa ni swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22107/ماذا-يفعل-من-يصلي-الراتبة-واقيمت-الصلاة
  • Imechapishwa: 26/10/2022