Alama inayokubaliwa na isiyokubaliwa kwenye kaburi

Swali: Kuweka waridi juu ya kaburi.

Jibu: Ni maovu na haijuzu. Lisipambwe na wala kusiwekwe waridi juu yake.

Swali: Kuweka alama juu ya kaburi.

Jibu: Alama haina neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kufa ´Uthmaan bin Madh´uun (Radhiya Allaahu ´anh) aliweka alama ili amtembelee. Akiweka alama ya jiwe, mbao au kitu mfano wake ni sawa.

Swali: Kuandika ni jambo limekatazwa?

Jibu: Hapana, haijuzu kuandika. Kusijengwe juu yake, kusikaliwe juu yake wala kusiandikwe juu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza yote hayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22108/حكم-وضع-العلامة-والورد-والكتابة-على-القبر
  • Imechapishwa: 26/10/2022