Maana ya Allaah kuwa mbinguni (في السماء):

Maana sahihi ya kwamba Allaah yuko mbinguni ni kwamba Allaah (Ta´ala) yuko juu ya mbingu. Maana ya في ni على juu na haina maana kwamba yuko ndani ya mbingu. Kwa sababu mbingu haimzunguki Allaah. Mtu anaweza kusema pia kuwa maana yake ni kwamba Yuko juu. Mbingu maana yake ni juu na haina maana ya mbingu iliyojengwa.

Tanbihi!

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah)  ametaja kuwa imenakiliwa kutoka katika baadhi ya vitabu vya kale kwamba miongoni mwa alama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake ni kwamba wanasujudu juu ya ardhi na wanadai kuwa Mola wao yuko mbinguni. Nukuu hii si sahihi. Haina mashiko. Isitoshe kuamini uwepo juu wa Allaah na kumsujudia Kwake sio kitu maalum kwa Ummah huu. Haisihi kufanywa alama kitu ambacho sio maalum. Jengine kuabiri ´madai` katika mazingira haya sio kusifu. Mara nyingi hutumiwa neno kudai katika jambo ambalo mtu ana mashaka nalo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 68
  • Imechapishwa: 26/10/2022