39. Maneno ya Imaam Maalik kuhusu kulingana kwa Allaah

Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Imaam Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah) aliulizwa:

“Ee Abu ´Abdillaah!

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

Amelingana namna gani?” Akajibu:

“Kulingana kunajulikana na namna haijulikani. Kuamini hilo ni wajibu na kuulizia hilo ni Bid´ah.” Kisha akaamrisha mtu yule atolewe nje.”[2]

MAELEZO

Jibu la Imaam Maalik bin Anas bin Maalik… baba yake siye Anas bin Maalik ambaye ni Swahabah. Ni watu wawili tofauti. Babu yake Maalik alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa Maswahabah na baba wa babu yake alikuwa ni miongoni mwa Maswahabah. Maalik alizaliwa mwaka wa 93 Madiynah na alifariki mwaka wa 179. Hapa ilikuwa ni katika zile zama za wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah.

Imaam Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah) aliulizwa:

“Ee Abu ´Abdillaah!

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]

Amelingana namna gani?” Akajibu:

“Kulingana kunajulikana na namna haijulikani. Kuamini hilo ni wajibu na kuulizia hilo ni Bid´ah.” Kisha akaamrisha mtu yule atolewe nje.”

Kulingana kunajulikana maana yake – Maana yake ni kuwa juu na kuthibiti na kutulizana.

Namna haijulikani maana – Ni kitu kisichotambulika kwa kutumia akili. Allaah (Ta´ala) ni Mkuu na Mtukufu zaidi kutokana na akili kutambua namna zilivyo sifa Zake.

Kuamini hilo ni wajibu – Kwa sababu ni kitu kilichopokelewa katika Qur-aan na Sunnah.

Kuulizia hilo ni Bid´ah – Kwa sababu kuuliza juu ya kitu hicho ni jambo halikuwepo wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.

Kisha akaamrisha muulizaji yule atolewe nje ya msikiti kwa kuchelea asije kuwafitinisha wengine katika ´Aqiydah na kumtia adabu kwa kumzuia kutokamana na vikao vya elimu.

[1] 20:05

[2] al-Bayhaqiy katika ”Kitaab-ul-Asmaa´ was-Swifaat” (867) na (868), na ad-Daarimiy katika “ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah” (104), al-Laalakaa´iy (664) na wengine.

[3] 20:05

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 26/10/2022