Swali: Kuna mlinganizi anayesema kuwa mtu anatakiwa kumfanya Allaah ndiye wa kwanza katika maisha yake, ajishughulishe na Allaah na kwamba mtu amfanye Allaah ndiye wa kwanza katika mambo yake yote muhimu na katika mawazo yake. Je, maelezo yake ni sahihi?

Jibu: Anakusudia kuwa amchunge Allaah. Aeleze kwa matamshi bora zaidi. Aseme amchunge Allaah na atahadhari na ghadhabu Zake. Aweke wazi kwamba mtu amchunge Allaah.

Swali: Hakuna makosa yoyote kusema kwamba mtu ajishughulishe na Allaah?

Jibu: Maana iko wazi. Anakusudia ajishughulishe na Allaah kwa kumtii na kuacha kumuasi.

Swali: Ni matamko yanayofaa?

Jibu: Sijui kama yana makosa yoyote. Lakini akiweka wazi zaidi ndio bora. Akibainisha kwa kusema mtu amchunge Allaah, ajihadhari na ghadhabu Zake na kumuasi, abainishe zaidi na wazi zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23309/حكم-التعبيرات-الموهمة-والملتبسة-في-الوعظ
  • Imechapishwa: 24/12/2023