09. Hadiyth “Swalah ya mwanamke inayopendeza zaidi kwa Allaah… “

348 – Ibn Khuzaymah ameipokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Ibraahiym al-Hijriy, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwake, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

إنَّ أحبَّ صلاةِ المرأة إلى الله في أشد مكانٍ في بيتها ظلْمة

“Swalah ya mwanamke inayopendeza zaidi kwa Allaah ni katika maeneo palipo na giza zaidi katika nyumba yake.”

Katika moja ya mapokezi yake mengine amesema[1]:

[إنّما] النساءُ عورةٌ، وإنَّ المرأَةَ لَتَخرجُ مِن بيتها وما بها بأسٌ، فَيَسْتَشْرِفُها الشيطانُ، فيقول: إنكِ لا تَمُرِّين بأحد إلا أعجبْتِهِ، وإنّ المرأة لتلبسُ ثيابَها، فيقال: أين تُريدين؟ فتقولُ: أعود مريضاً، أو أشهدُ جنازةً، أو أصلّي في مسجدٍ! وما عَبَدَتْ امرأةٌ ربَّها مثلَ أنْ تعبدَه في بَيتها

“Hakika mambo yalivyo ni kwamba wanawake ni uchi. Wakati mwanamke anapotoka nyumbani kwake pasi na udhuru, basi shaytwaan humfuatishia macho na kusema: “Hakika wewe hutompitia yeyote isipokuwa utampendeza.” Wakati mwanamke anapovaa nguo zake huulizwa ni wapi anapotaka kwenda, akajibu: “Humtembelea mgonjwa, kushiriki katika mazishi au kuswali msikitini.” Mwanamke hajamwabudu Mola Wake vyema zaidi kama anavyomwabudu katika nyumba yake.”[2]

Cheni ya wapokezi ni nzuri.

Kusema kuwa shaytwaan humfuatishia macho maana yake ni kwamba anamuinua, anamnyanyulia macho yake na anakuwa na hamu juu yake, kwa sababu amefanya jambo linalofanya aweze kumtawala, nalo ni kutoka katika nyumba yake[3].

[1] Bi maana Ibn Mas´uud, kama ilivyobainishwa katika “al-Mu´jam al-Kabiyr”. Kwa hivyo ni maneno ya Swahabah.

[2] Swahiyh kama maneno ya Swahabah.

[3] Hili ni kuhusu mashaytwaan wa kijini, kusemwe nini juu ya mashaytwaan wa kibinadamu? Khaswa mashaytwaan wa kibinadamu wa leo ambao wana madhara zaidi kwa mwanamke kuliko mashaytwaan elfu moja wa kijini. Kwa sababu vijana wengi wa leo hawana muruwa, dini, utukufu wala utu na kwa ajili hiyo wanamshambulia mwanamke kwa njia ya kutisha mno, jambo linalofahamisha uduni, unyonge na uharibifu. Kwa ajili hiyo ni juu ya watawala wa kiislamu kuhakikisha wanawatia adabu watenda madhambi hawa wabaya  na wanyama wakali wenye madhara.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/261)
  • Imechapishwa: 25/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy