Wanashuhudia na kuitakidi kuwa Maswahabah bora wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan na kisha ´Aliy, na kwamba wao ndio makhaliyfah waongofu ambao ukhaliyfah wao umetajwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale yaliyosimuliwa na Sa´iyd bin Jamhaan, kutoka kwa Safiynah, nayo ni:

”Ukhaliyfah baada yangu ni miaka thelathini.”[1]

Baada ya siku zao kwisha jambo lilirudi kwenye ufalme unaouma kwa mujibu wa yale aliyokhabarisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

[1] Abu Daawuud (4646) na at-Tirmidhî (2226). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3257).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 289-290
  • Imechapishwa: 24/12/2023