Kumchinjia mgeni au ndugu ni shirki?

Swali: Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni haramu na shirki. Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu ya kumchinjia mgeni au ndugu?

Jibu: Kuchinja kwa ajili ya kujikurubisha kwa yule unayemchinjia, kwa ajili ya kuleta manufaa na kuzuia madhara, ni shirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.

Ama kuhusu kuchinja kwa jina la Allaah (Ta´ala) kwa ajili ya kumlishiza mgeni au ndugu ni sawa.

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/129)
  • Imechapishwa: 06/10/2020