Hadiyth ya kipofu ni dalili ya kujuzu kuwaomba maiti?

Swali: Kuna hujuma nyingi kwa Salafiyyuun na kwamba ni watu wapingaji na hawawapendi mawalii. Miongoni mwa dalili walizotumia juu ya kwamba kuomba uokozi kwa maiti inajuzu ni ile Hadiyth ya mtu kipofu aliyeomba uokozi kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kufa kwake. Nimejua kuwa Hadiyth hii ni Swahiyh jambo ambalo limesababisha kwa baadhi ya watu kuwafanya kuwa na ghera kubwa. Naomba kufaidika kwa jambo hili muhimu.

Jibu: Baada ya kamati ya wanachuoni kudurusu imejibu kuwa Hadiyth ya kipofu imepokelewa na Imaam at-Tirmidhiy kwa mlolongo wake kupitia kwa ´Uthmaan bin Haniyf (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa kuna kipofu aliyekuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia:

”Niombee kwa Allaah aniponye.” Akamwambia: ”Ukipenda nitaomba na ukipenda kuwa na subira na ni bora kwako.” Akamwambia: ”Niombee.” Akamwamrisha atawadhe vizuri na aombe kwa du´aa hii:

”Ee Allaah! Hakika mimi ninakuomba na ninaelekea Kwako kupitia Mtume Wako Muhammad, Mtume wa Rahmah. Mimi nimeelekea kwako nikimwomba Mola Wangu kwa haja yangu ili anitatulie. Ee Allaah! Niponye kwaye.”

at-Tirmidhiy amesema kuwa Hadiyth ni Hasan Swahiyh Ghariyb. Hatuijui isipokuwa kwa sura hii tu kupitia Hadiyth ya Abu Ja´far al-Khitwamiy.

Tukikadiria kuwa ni Swahiyh hakuna dalili ya kipofu kumuomba du´aa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth inaonesha kuwa kipofu alimuomba Allaah (Ta´ala) kwa kumwelekea kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati ambapo alikuwa bado yuko hai kama jinsi alivyomuomba Allaah (Ta´ala) amtatulie haja zake kupitia du´aa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Katika Hadiyth hii hakuna kitu kinachotolea dalili kufahamisha kuwa inajuzu kuwaomba maiti. Abul-´Abbaas Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amezungumza kuhusu Hadiyth hii maneno mazuri katika kitabu kinachoitwa ”Qaa´idat-ul-Jaliylah fiy at-Tawassul wal-Wasiylah.” Rejea kitabu hicho ili ustafidi zaidi.

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/58)
  • Imechapishwa: 06/10/2020