Swali: Je, inafaa kuwapiga watoto usoni ili kuwatia adabu au kwa kutumia pasi?

Jibu: Ni lazima kuwatia adabu watoto. Si kwamba inafaa. Ni lazima hata kama watakuwa mayatima. Hata mayatima wanatiwa adabu wanapokosea. Wanatiwa adabu kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waamrisheni watoto wenu swalah wanapofikisha miaka saba na wapigeni kwayo wanapofikisha miaka kumi.”

Mtoto wa kiume au wa kike anapoacha swalah baada ya miaka kumi anachapwa. Anapokuwa ni mwenye mdomo mchafu anapigwa na kutiwa adabu. Ikiwa kuzungumza naye hakusaidii na ikiwa anapingana na kuwadhuru familia yake basi ni sawa akatiwa adabu mpaka anyooke. Ni mamoja ni yatima, mvulana, msichana, yatima au asiyekuwa yatima. Ikiwa kuzungumza kunasaidia ni vizuri. Vinginevyo atiwe adabu na mama yake, baba yake na kaka yake mkubwa mpaka anyooke. Akiachwa juu ya hali yake mpaka atakulia juu yake na hatimaye atakuwa ni madhara katika jamii. Lakini pale ambapo baba yake, mama yake na ndugu zake wakubwa watasimama dhidi yake, wakamwelekeza, wakamfunza na kumkataza kutokana na sifa mbaya kukiwemo kutusi, kusema uwongo, haswali baada ya kufikisha miaka kumi na mfano wa hayo, basi wamtie adabu mpaka akome ikiwa kuzungumza naye hakukumsaidia kitu wala kumuathiri.

Baadhi ya watu wanasema kuwa yatima haambiwi kitu. Ni kosa. Yatima akiachwa juu ya hali yake itakuwa mbaya tabia yake na matendo yake na hivyo atakulia juu ya shari. Hayo hayatokani na manufaa yake. Ni lazima kwa mlezi wa yatima amtie adabu kwa kumchapa ikiwa maneno hayakumnufaisha. Lakini asipige uso. Apige sehemu nyingine kusikokuwa uso kama vile mapacha, mgongo na mabega. Apige zile sehemu ambazo si khatari. Asipige uso kwa hali yoyote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kupiga uso. Vilevile asipige zile sehemu khatari. Lakini ampige zile sehemu zinazowezekana kama mfano wa makalio yake, mapaja yake na mgongo wake kichapo chepesi ambacho kitamzuia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4343/حكم-ضرب-او-كي-الاطفال-للتربية-والتاديب
  • Imechapishwa: 17/06/2022