Kumbeba mtoto wakati wa swalah kunapingana na unyenyekevu?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumbeba Umaamah kunapingana na unyenyekevu?

Jibu: Hakupingani na unyenyekevu muda wa kuwa mswaliji anaweza na hajikakami. Isitoshe kufanya hivo ni dalili na ili kuwafunza watu jambo hilo. Ni kama ambavo aliswali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya mimbari na akashuka ili awafunze watu kwamba jambo kama hilo haliitii swalah kasoro.

Swali: Vipi kuhusu yale yaliyopokelewa kwamba kutikisika mara tatu kunaharibu swalah?

Jibu: Hapana. Baadhi ya mapokezi hayana kikomo maalum. Hata hivyo mtu anatakiwa kufanya unyenyekevu na asicheze. Kumbeba au kumtua chini sio jambo linalofanywa kwa kufuatanisha. Alifanya hivo kwa ajili ya manufaa ya swalah kwa ajili ya kubainisha na kufunza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23934/هل-حمل-الطفل-في-الصلاة-ينافي-الخشوع
  • Imechapishwa: 01/08/2024