Dada wa kunyonya anaona aibu kukaa na ndugu yake

Swali: Vipi ikiwa nimemjua ndugu yangu wa kunyonya baada ya wasichana wameshakuwa wakubwa.

Jibu: Haijalishi kitu. Ikishatambulika tu basi.

Swali: Je, wanapata dhambi ikiwa aibu itawazuilia?

Jibu: Udhahiri ni kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Mpe idhini, kwani huyo ni ami yako.”

Asende kinyume na Shari´ah. Ikiwa yuko na aibu basi akae naye wakiwa na mtu mwingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23923/حكم-امتناع-المراة-عن-اخيها-من-الرضاعة
  • Imechapishwa: 01/08/2024