Swali: Kuna mtu amekufa akifa akiwa na deni na hakuacha mtu awezaye kumlipia nalo. Je, inafaa kulipa deni hilo kutoka katika pesa ya zakaah?

Jibu: Haijuzu kulipa deni la maiti kutoka katika pesa ya zakaah. Lakini kama alilichukua kwa nia ya kulipa baadaye basi Allaah atamlipia nalo.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/377)
  • Imechapishwa: 26/04/2026