Kulewa, kisha baadaye kujihisi vibaya – faida iko wapi?

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa pombe ina manufaa na kwa ajili hiyo wanainywa. Ni manufaa gani hayo yaliyomo ndani yake?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا

”Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na manufaa [fulani] kwa watu; na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemuomba Allaah aondoshe manufaa ya pombe hata kwa lengo la kujitibu. Amesema:

“Allaah asimponye.”

Pombe ni ugonjwa na si dawa. Pombe ina madhara mengi. Kuna faida gani kupoteza akili kwa muda na kisha kuamka ukiwa katika hali mbaya?

[1] 2:219

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 273
  • Imechapishwa: 14/04/2025