Nukuu za wazi kuharamisha pombe

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kuwa pombe sio haramu kwa sababu Allaah hakuteremsha Aayah inayotamka waziwazi kwamba ni haramu, alichosema ni:

فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

”… hivyo basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.”?[1]

Jibu: Jumla inayosema “jiepusheni” ni yenye nguvu zaidi kuliko kusema kuwa ni haramu. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) ameharamisha pombe. Yule mwenye kufikiwa na Aayah hii na akawa yuko na pombe, basi asiinywe wala asiiuze.”[2]

Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ameilaani pombe na mwenye kuinywa, mwenye kuihudumia, mwenye kuiuza, mwenye kuinunua, mwenye kuitengeneza, mwenye kutengenezewa, mwenye kuoda na kula thamani yake.”[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pale anapokunywa hali ya kuwa ni muumini na wala hapori kitu, jambo linalofanya watu kumuinulia macho, hali ya kuwa ni muumini.”[4]

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمْ عَنْهُ فَٱنتَهُوا۟ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni. Mcheni Allaah, hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[5]

Sentesi inayosema “jiepusheni” ni yenye nguvu zaidi kuliko kusema kuwa ni haramu.

[1] 5:90

[2] Muslim (1578).

[3] Abu Daawuud na al-Haakim. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5091).

[4] al-Bukhaariy (2475) na Muslim (57).

[5] 59:7

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 274
  • Imechapishwa: 14/04/2025