Allaah (´Azza wa Jalla) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيم

“Enyi mlioamini! Jieupusheni sana kuwa na dhana [mbaya], kwani hakika baadhi ya dhana ni dhamb, na wala msipelelezane na wala wasisengenyane baadhi yenu wengine. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa? Hivyo basi mmelichukia hilo, na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.”[1]

Kusengenya ni katika madhambi makubwa.

Kuna wafasiri wa Qur-aan waliyosema siku ya Qiyaamah ataletwa mtu ambaye uliyemsengenya na ataigizwa kwa kufanywa umbile lake akiwa maiti na baada ya hapo ataambiwa “Kula nyama yake”. Atalazimishwa kufanya hivo pamoja na kuwa ni jambo analolichukia. Atalazimishwa kuila ikiwa hii ndio adhabu kwake.

Kusengenya jambo ambalo ni kuvunja heshima ya ndugu yako ni haramu.

[1] 49:12

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/121)
  • Imechapishwa: 28/04/2024