Kula mpaka kuingie alfajiri ya kweli

Swali: Kulikuwa na kitambo gani kati ya daku na swalah ya Fajr?

Jibu: Wakati wa daku unatanda mpaka kuingia kwa alfajiri. Amesema (Ta´ala):

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi.”[1]

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bilaal anaadhini usiku. Hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Ibn Umm Maktuum alikuwa kipofu na haadhini mpaka aambiwe kuwa kumepambazuka. Kwa hivyo inapendeza kuchelewesha daku.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

[1] 02:187

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/334) nr. (5611)
  • Imechapishwa: 24/04/2022