Swali: Je, inafaa kufunga pasi na kula daku?

Jibu: Kilichosuniwa kwa mfungaji ni yeye kula daku kabla ya kupambazuka alfajiri. Kufanya hivo kunampa nguvu juu ya kufunga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amehimiza jambo hilo na akabainisha kuwa daku ina baraka. Lakini mtu akifunga bila kula daku swawm yake ni sahihi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/26) nr. (14093)
  • Imechapishwa: 24/04/2022