Swali: Ni ipi hukumu ya kukusanyika sehemu maalum wakati anapofariki mtu kwa muda wa siku tatu pamoja na kufanya walima kwa hoja ya kwamba walima huu hauhusiani na kilio, bali unahusiana na watu waliopo pale kilioni?

Jibu: Alikufa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ni kiumbe bora na wala Maswahabah hawakukusanyika kwenye nyumba na wala hawakufanya walima. Abu Bakr alikufa, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Maswahabah bora, waliokuja baada yao na wanachuoni na wala hakukuthibiti ya kwamba Waislamu walikusanyika kwenye nyumba, si siku moja wala siku tatu. Kwa kuwa hili ni katika ukalifisho ambao watu wenyewe wamejikalifisha. Kusifanywe walima wala kitu kingine chochote.

Kutoa pole ni jambo limewekwa, lakini isiwe kwa njia hii. Mtu anaweza kutoa pole kwa kumuombea du´aa:

أَحْسَـنَ الله عَـزاءَ كَ و جبر الله مصيبتك وَغَفَـرَ لِمَـيِّتِكَ

“Allaah akufanye kuzuri kutaaziwa kwako, aunge msiba wako na amsamehe maiti wako.”

Haya ndio unatakiwa kumwambia, sawa kwa njia ya kukutana, kwa njia ya simu au ukamtumia barua. Hakuna haja ya kukusanyika na wala hakuna haja ya kufanya walima.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12537
  • Imechapishwa: 24/09/2020