al-Fawzaan kuhusu dawa iliyo na alcohol

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia dawa ambayo ina asilimia kidogo ya alcohol?

Jibu: Ikithibiti kuwa ndani yake kuna asilimia ya alcohol – bi maana pombe, alcohol ni pombe – ikithibiti kuwa ndani yake kuna alcohol hata kama ni asilimia kidogo ya pombe, basi itakuwa ni haramu kwake kuitumia. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“… basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.” (05:90)

Akasema kuhusiana na pombe:

إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Hakika si vyenginevyo ulevi na kamari na masanamu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli ni uchafu katika matendo ya shaytwaan; hivyo basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.” (05:90)

Mtu anatakiwa kujiepusha na pombe sawa ikiwa ndogo au nyingi, ni mamoja ikiwa ni katika dawa, chakula na kinywaji, mtu ajiepushe na pombe kwa kuwa ni uchafu katika matendo ya shaytwaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12537
  • Imechapishwa: 24/09/2020