Swali: Ni ipi hukumu ya kukusanya michango juu ya vituo na masomo yasiyofuata mfumo wa Salaf?

Jibu: Haijuzu kushirikiana na watu wanaokusanya michango kwa ajili ya kufungua jumuiya za kizushi, kikhurafi na za batili. Hilo ni haramu. Haijuzu kushirikiana nao khaswa katika jambo hilo. Hata hivyo hapana vibaya na ni jambo linatakikana kushirikiana nao katika kuwanufaisha na kuwasaidia waislamu, muda wa kuwa hawatokuwekea chochote katika sharti zao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema hata juu ya makafiri:

“Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Hawatoniomba jambo ambalo lina kutukuza amri ya Allaah, isipokuwa nitawaitikia.”[1]

Hata hivyo ni haramu na haijuzu kukusanya michango kwa ajili ya kujenga msikiti juu ya makaburi, taasisi za kivyamavyama na mfano wa hayo.

[1] al-Bukhaariy (2731).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/samla-pengar-till-moskeer-som-inte-rattar-sig-efter-salafs-metodik/
  • Imechapishwa: 01/10/2023