Makosa yasiyo na maana yanayoelekezwa katika Sharh-us-Sunnah al-Barbahaariy

Swali: Wanapoambiwa baadhi ya watu kwamba wanazuoni wanapendekeza Sharh-us-Sunnah ya al-Barbahaariy, wanaanza kuuliza maswali ya kutia shaka kama kweli kitabu hicho kimethibiti kuandikwa na mtunzi. Aidha wanasema kuwa kitabu hicho ni tatizo kwa sababu ya maneno ya al-Barbahaariy aliposema:

”Mwenye kukubaliana na kitabu hichi, akakiamini na akakifanya kuwa ni kiigizo chema na wala asitilie shaka na kukanusha herufi yake hata moja, ni mtu wa Sunnah na Jamaa´ah. Ni mkamilifu, kwa sababu Sunnah imekamilika kwake. Ambaye atakanusha, kutilia shaka herufi moja ya kitabu hichi au akajitenga ni mtu wa matamanio.”[1]

Kwa sababu ndani ya kitabu kuna mambo pia ya ki-Fiqh, kama vile kupangusa juu ya soksi za ngozi. Unasemaje juu ya wenye kuchukua msimamo huu juu ya Sharh-us-Sunnah ya al-Barbahaariy?

Jibu: Alisema nini kuhusu kufuta juu ya soksi za ngozi? Ameenda kinyume na Sunnah? al-Barbahaariy hakwenda kinyume na Sunnah katika suala linalohusu kupangusa juu ya soksi za ngozi. Haya ni maneno ya upuuzi yasiyokuwa na maana yoyote. Ni maneno yasiyo na maana.

[1] Sharh-us-Sunnah (166).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/vardelos-anmarkning-pa-al-barbaharis-sharh-us-sunnah/
  • Imechapishwa: 01/10/2023