Swali 35: Alitoka akahajiri (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) namna gani? Ni nani alihajiri pamoja naye?

Jibu: Alitoka yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Abu Bakr kwenda katika pango la Thawr. Wakakubaliana na mwelekeza njia wao kuja na vipandwa vyao baada ya siku tatu kwenye pango. Walipokuwa pangoni washirikina wakaanza kuwatafuta. Mwishowe wakafika mpaka kwenye pango ambapo Allaah akawapofosha macho yao. Unafikiria nini juu ya watu wawili ambao watatu wao ni Allaah? Baada ya kupita siku tatu na ikatulia kidogo sakata la kuwatafuta, mwelekeza njia akaja na vipandwa vyao. Wakawapanda. Walipokuwa njiani Sarraaqah bin Maalik bin Ja´tham akawawahi. Aliposogea karibu nao, farasi wake akakwama kwenye matope na ikambidi kuwaomba hifadhi. Wakampa hifadhi baada na yeye kuwafichia safari yao.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 01/10/2023