Kukusanya miguu wakati wa Sujuud

Swali: Je, inafaa kuleta miguu pamoja wakati wa kusujudu?

Jibu: Hapana, aiinue na kuitenganisha. Hili ndilo lililohifadhiwa katika Sunnah. Ama kuhusu upokezi wa Ibn Khuzaymah na al-Haakim zinahitaji kuangaliwa vyema… zina udhaifu. Miguu inapaswa kuinuliwa, hivo ndio bora zaidi. Kama ilivyopokewa katika upokezi wa Muslim.

Swali: Je, aitenganishe?

Jibu: Ndio, inapaswa kuinuliwa na kutenganishwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24846/ما-حكم-ضم-القدمين-عند-السجود
  • Imechapishwa: 20/12/2024