Sentesi ”Katika ulimwengu kote” wakati wa kumswalia Mtume

Swali: Vipi kuhusu sentesi:

في العالمين إنك حميد مجيد

”… katika ulimwengu kote. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”

Jibu: Hii ni wakati wa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), si katika Tashahhud. Hapana vibaya akisema hivo. Imepokelewa katika upokezi wa Ibn Mas’uud:

اللهم صل على محمد [النبي الأمي]و على آل محمد كما صليت على [آل]إبراهيم، و بارك على محمد [النبي الأمي]و على آل محمد كما باركت على [آل]إبراهيم في العالمين، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad [Mtume ambaye si msomi] na jamaa zake Muhammad kama Ulivyowasifu [jamaa za] Ibraahiym. Mbariki Muhammad [Mtume ambaye si msomi] na jamaa zake Muhammad kama Ulivyowabariki [jamaa za] Ibraahiym katika ulimwengu kote. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

[1] Muslim, Abu ´Awaanah, Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Muswannaf” (1/132/2), Abu Daawuud na an-Nasaa’iy (159-161). Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24856/حكم-زيادة-في-العالمين-في-التشهد
  • Imechapishwa: 20/12/2024