Kukufuru kunaweza kuwa kwa moja kati ya mambo matatu

Swali: Mwenye kusema kwamba hakufuru mtu mpaka akusudie kutoka nje ya Uislamu kwa maneno au matendo yake?

Jibu: Huyu ni mjinga. Afundishwe kwamba kufuru inaweza kuwa kwa moyo, mdomo au matendo. Wale waliosema:

“Hatujawaji kuona mfano wa wasomaji wetu hawa.”[1]

walikufuru kwa maneno.

Swali: Mwenye kusema hivi anakuwa Murji-ah?

Jibu: Murji-ah wanaona kinyume na hivi. Wanaona kuwa imani inakuwa kwa moyo na kwa mdomo. Lakini hawaoni kuwa haya hayaitwi ´imani`. Wanaona kuwa swalah na zakaah ni wajibu. Lakini haviitwi kuwa ni ´imani`. Hili ni kosa.

[1] at-Twabariy (10/172).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 135
  • Imechapishwa: 16/09/2019