Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah wanawake kucheza dufu katika harusi, je, inajuzu vilevile kukodisha wanawake kwa ajili ya hilo?
Jibu: Ndio, inajuzu. Kitendo hichi si kwamba kinajuzu tu bali kimewekwa vilevile katika Shari´ah. Inajuzu kuchukua ujira kwa vitu ambavyo vimewekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
“Allaah akiharamisha kitu, basi anaharamisha vilevile thamani yake.”
Chukua kanuni mbili kutoka kwenye Hadiyth hii:
1- Akiharamisha kitu, Anaharamisha vilevile thamani yake.
2- Akihalalisha kitu, Anahalalisha vilevile thamani yake.
Pamoja na kwamba inajuzu kuajiri mwanamke mwenye kucheza dufu. Hata hivyo thamani lazima iwe mantiki. Kupewa 1,523 $ kwa sababu ya kucheza saa moja au mbili tu si sahihi. Ni kupetuka mipaka na israfu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
- Imechapishwa: 21/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket