Mwanamke aolewe na mwanaume mzuri

Inapendekezwa kwa mababa ambao wanataka kuwaoza wasichana wao amtafutie mume mzuri. Mwanamke anataka kile ambacho mwanaume anataka. az-Zubayr bin al-‘Awaam (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Mnawaoza mabanati zenu kwa wanaume wabaya na waasi. Hakika wanataka yale mnayotaka.”[1]

‘Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Msimuoze mwanamke kwa mwanaume mbaya na muasi. Wanatamani yale mnayotamani.”

[1] ´Abdur-Razzaaq i ”al-Muswannaf” (10339).

Check Also

Kaoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab ambaye hataki kuingia katika Uislamu

Swali: Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab kabla ya kuwa na msimamo, na nimepewa fatwa na baadhi …